• HABARI MPYA

  Tuesday, June 25, 2024

  KIBU D ‘MKANDAJI’ MALI YA SIMBA SC HADI 2026


  KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Kibu Denis Prosper (25) amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya Simba hadi mwaka 2026.
  Anakuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa leo amesaini mkataba mpya baada ya beki 
  Israel Patrick Mwenda (24) na kiungo, Mzamiru Yassin Selemba (28) ambao wote wameongeza mikataba ya miaka miwili kila mmoja hadi mwaka 2026.
  Na hiyo inafuatia Simba SC kuacha wachezaji sita hadi sasa ambao ni mabeki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.
  Aidha, tayari Simba SC imemtambulisha mchezaji mmoja tu mpya, beki chipukizi wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIBU D ‘MKANDAJI’ MALI YA SIMBA SC HADI 2026 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top