• HABARI MPYA

  Wednesday, June 12, 2024

  BIASHARA UNITED YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 MUSOMA


  TIMU ya Biashara United imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza Ligi Kuu msimu ujao leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Herbert Lukindo kwa penaltı dakika ya 90’+9 na timu hizo zitarudiana Jumapili Uwanja wa  Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora na mshindi wa jumla atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
  Biashara United imetoka Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza kwa kuifunga 2-0 nyumbani na ugenini, wakati Tabora United imeporomoka Ligi Kuu ya kufungwa kwa jumla ya mabao 4-0 na JKT Tanzania, 4-0 Tabora na 0-0 Mbweni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top