• HABARI MPYA

  Sunday, June 16, 2024

  ‘MADOGO’ WA YANGA WACHAPA ‘SIMBA MTOTO’ 2-1 CHAMAZI


  TIMU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na Chitunzi Masaka dakika ya 64 na Hamisi Iddi dakika ya 67, wakati bao pekee la Simba limefungwa na Athumani Iddi dakika ya 61.
  Katika mchezo uliotangulia mchana Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania bao pekee la Rashid Abdallah hapo hapo Azam Complex.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘MADOGO’ WA YANGA WACHAPA ‘SIMBA MTOTO’ 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top