• HABARI MPYA

  Sunday, June 02, 2024

  NI YANGA SC WASHINDI KOMBE LA CRDB, WAIUA AZAM KWA MATUTA  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayojulikana kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa penaltı 6-5 dhidi ya Azam FC 
  kufuatia sare ya bila mabao ndani ya dakika 120 usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
  Zilikuwa dakika 120 za patashika haswa, Azam FC wakitawala kipindi cha kwanza na Yanga kipindi cha pili wakati kwenye dakika 30 za nyongeza timu hizo zilishambuliana kwa zamu.
  Waliofunga penaltı za Yanga ni nyota wa Ivory Coast, kiungo Peodoh Pacome Zouzoua, beki Kouassi Attohoula Yao, beki mzawa na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto, kiungo Mganda Khalid Aucho, mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda na kiungo mzawa, Jonas Gerald Mkude.
  Waliokosa uoande wa Yanga ni kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Gnadou Guerde ambao mikwaju yao iliokolewa na kipa Msudan, Mohamed Mustafa na beki mzawa, İbrahim Hamad ‘Bacca’ aliyepaisha juu.
  Waliofunga penaltı za Azam FC ni kiungo mzawa, Adolph Mutasingwa Bitebeko, beki Msenegal, Cheikh Sidibé, winga Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon, beki mzawa, Edward Charles Manyama na kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah.
  Waliokosa ni beki Mcolombia Yeison Fuentes Mendoza aliyegongesha mwamba, winga Mgambia, Gibril Silah na beki mzawa Lusajo Mwaikenda ambao mikwaju yao iliokolewa na Kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra na winga mzawa Iddi Suleiman ‘Nado’ aliyepiga juu ya lango.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA SC WASHINDI KOMBE LA CRDB, WAIUA AZAM KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top