• HABARI MPYA

  Friday, June 28, 2024

  TABORA UNITED, BIASHARA UNITED ZATOZWA MAMILIONI


  KLABU za Tabora United na Biashara United zimetozwa Faini kwa makosa mbalimbali ikiwemo vurugu za mashabiki na ukiukaji wa kanuni katika mechi mbili baina yao, nyumbani na ugenini katikati ya mwezi huu.
  Ikumbukwe Tabora United ilinusurika kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United Juni 16 katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa mwisho wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Matokeo hayo yaliifanya Tabora United iitoe Biashara United kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Juni 12 Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Biashara United iliingia kwenye mchezo huo ikitokea ligi ya NBC Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza m na Tabora United ilitolewa na JKT Tanzania katika mchujo wa Ligi Kuu.
  GONGA KUSOMA TAARIFA KAMILI YA BODI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED, BIASHARA UNITED ZATOZWA MAMILIONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top