• HABARI MPYA

  Wednesday, June 19, 2024

  SHAABAN CHILUNDA NAYE AONYESHWA GETI LA KUTOKEA SIMBA SC


  MSHAMBULIAJI Shaaban Iddi Chilunda amekuwa mchezaji wa tatu kuachwa na klabu ya Simba SC baada ya kumalizika msimu ikishika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Chilunda (25) alijiunga na Simba SC mwanzoni mwa msimu akitokea Azam FC, lakini wakati wa dirisha dogo akatolewa kwa mkopo KMC.
  Anakuwa mchezaji wa tatu kuachwa baada ya aliyekuwa Nahodha John Raphael Bocco na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHAABAN CHILUNDA NAYE AONYESHWA GETI LA KUTOKEA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top