• HABARI MPYA

  Saturday, June 15, 2024

  WENYEJI UJERUMANI WAANZA KWA KISHINDO EURO 2024, YASHINDA 5-1


  WENYEJI, Ujerumani jana wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya 'Euro 2024' baada ya kuichapa Scotland mabao 5-1 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  Mabao ya 'Die Mannschaft' jana yalifungwa na kiungo wa Bayer Leverkusen, Florian Richard Wirtz dakika ya 10, mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala dakika ya 19 na kiungo wa Arsenal, Kai Lukas Havertz kwa penalti dakika ya 45'+1.
  Mabao mengine yalifungwa na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Niclas Fullkrug dakika ya 68 na kiungo wa Borussia Dortmund, Emre Can dakika ya 90'+3, wakati bao pekee la 'The Tartan Army' alijifunga beki wa Real Madrid, Antonio Rüdiger dakika ya 87.
  Mechi nyingine ya Kundi A leo, Uswisi imeifunga Hungary mabao 3-1 Uwanja wa RheinEnergie Jijini Cologne.
  Mabao yake yakifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Ghana, Kwadwo Antwi Duah dakika ya 12, kiungo Michel Aebischer dakika ya 45 na mshambuliaji mwenye asili ya Cameroon, Breel Donald Embolo dakika ya 90'+3, wakati bao pekee la Hungary limefungwa na Barnabás Varga dakika ya 66.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENYEJI UJERUMANI WAANZA KWA KISHINDO EURO 2024, YASHINDA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top