• HABARI MPYA

  Tuesday, June 04, 2024

  JKT TANZANIA YAICHAPA TABORA UNITED 4-0 PALE PALE MWINYI


  TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na viungo Said Hamisi Ndemla dakika ya tisa, İsmail Aziz ‘Kader’ dakika ya 20, mshambuliaji Matheo Anthony Simon dakika ya 81 na kiungo Hassan Dilunga dakika ya 90’+2.
  Tabora United sasa wanakabiliwa na mzigo wa kwenda kushinda ugenini mabao 5-0 Jumamosi Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam au ishinde 4-0 mshindi wa jumla apatikane kwa mikwaju ya penaltı abaki Ligi Kuu.
  Timu itakayopoteza kwa matokeo ya jumla Jumamosi itakwenda kumenyana na Biashara United ya Mara kutoka Championship kwa michezo mingine miwili ya nyumbani na ugenini kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA TABORA UNITED 4-0 PALE PALE MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top