• HABARI MPYA

  Tuesday, June 25, 2024

  ISRAEL PATRICK MWENDA AONGEZA MKATABA SIMBA SC


  BEKI Israel Patrick Mwenda (24) anayeweza kucheza kama kiungo mshambuliaji, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC hadi mwaka 2026.
  Anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa ameongeza mkataba baada ya kiungo, Mzamiru Yassin Selemba (28) ambaye pia ameongeza mkataba wa miaka miwili hadi mwaka 2026.
  Na hiyo inafuatia Simba SC kuacha wachezaji sita hadi sasa ambao ni mabeki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.
  Aidha, tayari Simba SC imemtambulisha mchezaji mmoja tu mpya, beki chipukizi wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ISRAEL PATRICK MWENDA AONGEZA MKATABA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top