• HABARI MPYA

  Wednesday, June 12, 2024

  MO DEWJI AAMUA KUURUDIA UENYEKITI WA BODI SIMBA, TRY AGAIN 'APUMZIKA'


  BILIONEA mwenye asili ya Kiasia, Mohamed ‘Mo Dewji’ amerejea kwenye Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba baada ya Salum Abdallah Muhene 'Try Again' kujiuzulu jana jioni.
  Mo Dewji ameposti video kwenye ukurasa wake Instagram akielezea azm yake ya kurejea kwa muda kwenye Uenyekiti wa Bodi ya Simba hadi hapo mambo yatakapokaa sawa na kuteuliwa Mwenyekiti mwingine.
  Mo Dewji alijiuzulu Uenyekiti wa Bodi Septemba 29, mwaka 2021 na kumteua aliyekuwa Makamu wake, Try Again kukaimu nafasi hiyo naye kubaki Rais wa Heshima wa klabu hiyo na mwekezaji pekee kwa umiliki wa asilimia 49 ya hisa zenye thamani ya Sh. Bilioni 20.
  VIDEO: MOHAMED ‘MO DEWJI’ AKIZUNGUMZA
  Februari 28, mwaka jana Mo Dewji alimteua tena Try Again kuendelea na Uenyekiti wa Bodi ya Simba akimteulia na Wajumbe wapya ambao ni Dk. Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.
  Hatua hiyo ilifuatia kufanyika uchaguzi mkuu uliomrejesha madarakani Mwenyekiti Murtaza Mangungu Januari 30, mwaka 2023 na Wajumbe Dk. Seif Ramadhan Muba, Asha Baraka, CPA Issa Masoud Iddi, Rodney Chiduo na Seleman Haroub. 
  Kwa upande wake, Try Again akitangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi alisema kwamba amemuomba Mo Dewji arejee kuwa Mwenyekiti wa Bodi, naye abaki kuwa mwanachama wa Simba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MO DEWJI AAMUA KUURUDIA UENYEKITI WA BODI SIMBA, TRY AGAIN 'APUMZIKA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top