// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HISPANIA YAWACHAPA MABINGWA ITALI NA KUSONGA MBELE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HISPANIA YAWACHAPA MABINGWA ITALI NA KUSONGA MBELE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2024

  HISPANIA YAWACHAPA MABINGWA ITALI NA KUSONGA MBELE


  TIMU ya Taifa ya Hispania imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Italia katika mchezo wa Kundi B usiku wa Alhamisi Uwanja wa Arena AufSchalke Jijini Gelsenkirchen nchini Ujerumani.
  Bao pekee la Hispania limefungwa na beki wa Bologna, Riccardo Calafiori aliyejifunga dakika ya 55 na kwa ushindi huo katika mchezo wa pili wanafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi B wakifuatiwa na Italia yenye pointi tatu, Albania moja sawa na Croatia.
  Mechi nyingine za Kundi C jana zote zilimalizika kwa sare ya 1-1 baina ya
  Slovenia na Serbia na Denmark dhidi ya England.
  Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, beki Žan Karničnik alianza kuifungia Slovenia dakika ya 69, kabla ya mshambuliaji wa AÇ Milan, Luka Jović kuisawazishia Serbia dakika ya 90’+5.
  Na Uwanja wa Waldstadion Jijini Frankfurt, Nahodha na mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Edward Kane alianza kuifungia England dakika ya 18, kabla ya kiungo wa Sporting CP ya Ureno, Morten Hjulmand kuisawazishia Denmark dakika ya 34.
  Msimamo wa Kundi C sasa ni England pointi kileleni wakifuatiwa na Denmark na Slovenia zenye pointi mbili kila moja, wakati Serbia yenye pointi moja inashika mkia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA YAWACHAPA MABINGWA ITALI NA KUSONGA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top