• HABARI MPYA

  Thursday, June 20, 2024

  UJERUMANI YASONGA KWENYE MTOANO EURO 2024


  WENYEJI, Ujerumani wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya  Hungary katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jumatano Uwanja wa MHPArena Jijini Stuttgart.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao ya ‘Nationalelf’, viungo wa Bayern Munich mwenye asili ya Nigeria, Jamal Musiala dakika ya 22 na İlkay Gündoğan wa Barcelona mwenye asili ya Uturuki dakika ya 67.
  Kwa ushindi huo, Ujerumani wanafikisha pointi sita pamoja na ushindi wa mechi ya kwanza wa 5-1 dhidi ya Scotland na wanajihakikishia kusonga mbele kwa  sababu timu pekee yenye uwezo wa kuzikatama pointi hizo ni Uswisi pekee baada ya sare ya 1-1 na Scotland usiku wa Jumatano.
  Nayo Croatia imetoka sare ya 2-2 na Albania katika mchezo uliotangulia wa Kundi B.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UJERUMANI YASONGA KWENYE MTOANO EURO 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top