• HABARI MPYA

  Thursday, June 20, 2024

  SIMBA SC YATAMBULISHA MKALI MPYA WA KWANZA, NI LAWI WA COASTAL


  KLABU ya Simba SC imemtambulisha beki wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga kuwa mchezaji wake wa kwanza mpya kuelekea msimu ujao.
  Na hiyo inafuatia kuacha wachezaji watano akiwemo beki wa katı, Kennedy Wilson Juma Ambasa (29) aliyedumu kikosini tangu Julai 2019 alipowasili kutoka Singida United.
  Wengine walioachwa Simba SC ni viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATAMBULISHA MKALI MPYA WA KWANZA, NI LAWI WA COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top