// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UJERUMANI YAMALIZA MECHI ZA KUNDI LAKE KWA SARE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UJERUMANI YAMALIZA MECHI ZA KUNDI LAKE KWA SARE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Monday, June 24, 2024

  UJERUMANI YAMALIZA MECHI ZA KUNDI LAKE KWA SARE


  WENYEJ, Ujerumani wamekamilisha mechi zao za Kundi A kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Uswisi usiku wa Jumapili Uwanja wa Frankfurt Arena Jijini Frankfurt.
  Mshambuliaji wa Bologna, Dan Assane Ndoye mwenye asili ya Senegal alianza kuifungia Uswisi dakika ya 28, kabla ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Niclas Füllkrug kuisawazishia Ujerumani dakika ya  90’+2.
  Ujerumani imemaliza na pointi saba kileleni ikifuatiwa na Uswisi pointi tano na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora, wakati Hungary iliyoifunga Scotland 1-0 jana bao la Kevin Csoboth dakika ya 90+10' ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu.
  Hungary inaweza kwenda Hatua ya 16 Bora kupitia Kapu la washindi wa pili bora, wakati Scotland safari yao imeisha hapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAMALIZA MECHI ZA KUNDI LAKE KWA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top