• HABARI MPYA

  Monday, June 17, 2024

  ENGLAND NA UHOLANZI ZAANZA VYEMA EURO 2024


  TIMU ya England imeanza vyema Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Serbia usiku wa jana katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa AufSchalke, Gelsenkirchen nchini Ujerumani.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Real Madrid, Jude Victor William Bellingham dakika ya 13 kwa kichwa baada ya krosi nzuri kutoka upande wa kulia.
  Mechi nyingine ya Kundi C jana  Slovenia ilitoka sare ya 1-1 na Denmark Uwanja wa MHPArena, Jijini Stuttgart .
  Kiungo wa Manchester United, Christian Dannemann Eriksen  alianza kuifungia Denmark dakika ya 17, kabla ya beki wa kishoto wa Górnik Zabrze ya Poland, Erik Janža kuisawazishia Slovenia dakika ya 77.
  Mechi moja ya Kundi D ilipigwa pia jana Uholanzi ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Poland Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg.
  Mabao ya Uholanzi yalifungwa na winga wa Liverpool, Cody Mathès Gakpo dakika ya 29 na mshambuliaji wa Burnley, Wout François Maria Weghorst dakika ya 83 baada ya mshambuliaji wa Antalyaspor, Adam Buksa kuanza kuifungia Poland dakika ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENGLAND NA UHOLANZI ZAANZA VYEMA EURO 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top