• HABARI MPYA

  Tuesday, June 18, 2024

  UFARANSA YASHINDA LAKINI MBAPPE AUMIA PUA NA KUTOLEWA NJE


  UFARANSA imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Austria katika mchezo wa Kundi D usiku wa Jumatatu Uwanja wa Merkur Spiel-Arena Jijini Düsseldorf nchini Ujerumani.
  Lilikuwa bao la kujifunga la beki wa kushoto wa Leeds United, Maximilian Wober dakika ya 38  lililoipa mwanzo mzuri Les Bleus na mbaya Austria katika Fainali za Euro 2024.
  Hata hivyo, Ufaransa ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Kylian Mbappe kuumia pua kufuatia kugongana na beki wa Lens ya Ufaransa, Kevin Danso na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji wa AÇ Milan, Olivier Giroud dakika ya 90.
  Katika mechi zilizotangulia za Kundi E, Romania iliichapa Ukraine 3-0, mabao ya viungo Nicolae Stanciu dakika ya 29, Răzvan Marin dakika ya 53 na mshambuliaji Denis Drăguș dakika ya 57 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, wakati Slovakia iliilaza Ubelgiji 1-0 bao la mshambuliaji Ivan Schranz dakika ya sana Uwanja wa Waldstadion Jijini Frankfurt.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YASHINDA LAKINI MBAPPE AUMIA PUA NA KUTOLEWA NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top