• HABARI MPYA

  Tuesday, June 11, 2024

  BOSI SIMBA AKUTANA KOCHA WA U17 JOHN BOCCO KWA MAJADILIANO


  AFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula jana alifanya kikao na Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, John Raphael Bocco juu ya maendeleo ya timu hiyo.
  Nahodha huyo wa Simba SC, Bocco (34) alicheza nusu ya kwanza tu ya msimu uliomalizika, kabla ya kuumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
  Alilikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba kwenye mechi ya kwanza ya Mapinduzi dhidi ya JKU Januari 1 mwaka huu Simba SC ikishinda 3-1 na akapangwa aanze mechi ya pili, bahati mbaya akaumia katika mazoezi ya kupasha misuli moto Januari 3 dhidi ya Singida Fountain Gate na ndio akamaliza msimu.
  Simba ilishinda 2-0 mechi hiyo ya Kundi B na kwenda Robo Fainali na wakafika hadi Fainali wakafungwa 1-0 na Mlandege Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOSI SIMBA AKUTANA KOCHA WA U17 JOHN BOCCO KWA MAJADILIANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top