• HABARI MPYA

  Sunday, June 02, 2024

  TAIFA STARS YATOKA SULUHU NA INDONESIA JAKARTA


  TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imetoka sare ya bila mabao na wenyeji, Indonesia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Madya Gelora Bung Karno Jijini Jakarta.
  Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji, Zambia Juni 11 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 ni Morocco, Zambia, Niger, Kongo na Eritrea ambayo imejitoa katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.
  Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Novemba 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la mshambuliaji mzaliwa wa DRC, Kokola Charles William M'Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.
  VIDEO: KOCHA WA TAIFA STARS, HEMED SULEIMAN MOROCCO AKIZUNGUMZA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YATOKA SULUHU NA INDONESIA JAKARTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top