• HABARI MPYA

  Tuesday, June 11, 2024

  MAZEMBE NA WABABE WA ZAMBIA WAJA KOMBE LA KAGAME ZANZIBAR


  TIMU za TP Mazemba (DRC), Nyasa Big Bullets FC (Malawi), na Red Arrows FC ya Zambia zitashiriki michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 6 hadi 22 Dar es Salaam na Zanzibar.
  Kuna jumla ya timu 15 zilizothibitisha kushiriki CECAFA Kagame Cup 2024, wakiwemo wenyeji JKU SC (Zanzibar), Simba SC, Yanga SC, Azam FC za Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga.
  Nyingine ni Gor Mahia (Kenya), Villa SC (Uganda), Vitalo'O (Burundi), APR FC (Rwanda), El Merreikh  (Sudan), Al Hilal  (Sudan), Hai El Waldi (Sudan) na El Merreikh FC-Bentiu (Sudan Kusini).
  Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika Dar es Salaam, Tanzania mwaka 2021 na Express FC ya Uganda ikaibuka bingwa kwa kuichapa Nyasa Big Bullets ya Malawi 1-0 kwenye fainali.
  CECAFA member associations include Kenya, Uganda, Tanzania, South Sudan, Sudan, Ethiopia, Eritrea, Zanzibar, Somalia, Rwanda, Burundi, and Djibouti.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE NA WABABE WA ZAMBIA WAJA KOMBE LA KAGAME ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top