// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HISPANIA NA ITALIA NAZO ZAANZA VYEMA EURO 2024 UJERUMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HISPANIA NA ITALIA NAZO ZAANZA VYEMA EURO 2024 UJERUMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, June 16, 2024

  HISPANIA NA ITALIA NAZO ZAANZA VYEMA EURO 2024 UJERUMANI


  TIMU ya Hispania jana imeanza vyema Kombe la Mataifa Ulaya 'Euro 2024' baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Croatia katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Olympia Jijini Berlin.
  Mabao ya La Roja yalifungwa na mshambuliajiwa wa Atletico Madrid, Álvaro Morata dakika ya 29, kiungo wa PSG, Fabián Ruiz damika ya 32 na beki wa Real Madrid, Dani Carvajal dakika ya 45'+2.
  Mechi nyingine ya Kundi B jana, mabingwa watetezi, Italia waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Albania Uwanja wa BVB Jijini Dortmund.
  Mabao ya 'Gli Azzurri' yote yalifungwa nyota wa Inter Milan, beki Alessandro Bastoni dakika ya 11 na kiungo Nicolò Barella dakika ya 16, wakati la Albania lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Sassuolo ya Italia, Nedim Bajrami dakika ya kwanza.
  Katika mchezo uliotangulia wa Kundi A jana jioni, Uswisi iliifunga Hungary mabao 3-1 Uwanja wa RheinEnergie Jijini Cologne.
  Mabao ya Uswisi yalifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Ghana, Kwadwo Antwi Duah dakika ya 12, kiungo Michel Aebischer dakika ya 45 na mshambuliaji mwenye asili ya Cameroon, Breel Donald Embolo dakika ya 90'+3, wakati bao pekee la Hungary limefungwa na Barnabás Varga dakika ya 66. 
  Ikumbukwe katika mechi ya ufunguzi juzi, wenyeji, Ujerumani walianza vyema baada ya kuichapa Scotland mabao 5-1 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  Mabao ya 'Die Mannschaft' jana yalifungwa na kiungo wa Bayer Leverkusen, Florian Richard Wirtz dakika ya 10, mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala dakika ya 19 na kiungo wa Arsenal, Kai Lukas Havertz kwa penalti dakika ya 45'+1.
  Mabao mengine yalifungwa na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Niclas Fullkrug dakika ya 68 na kiungo wa Borussia Dortmund, Emre Can dakika ya 90'+3, wakati bao pekee la 'The Tartan Army' alijifunga beki wa Real Madrid, Antonio Rüdiger dakika ya 87. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA NA ITALIA NAZO ZAANZA VYEMA EURO 2024 UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top