• HABARI MPYA

  Monday, June 03, 2024

  ADOLF MTASINGWA AONGEZWA KIKOSI CHA TAIFA STARS MECHI NA ZAMBIA


  KIUNGO wa Azam FC, Adolf Mtasingwa Bitegeko (25) ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji, Zambia Juni 11 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  Mchezaji huyo ameongezwa Taifa Stars baada ya kuonyesha kiwango kizuri siku za karibuni katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na jana kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayojulikana kama CRDB Bank Federation Cup Azam FC Ikifungwa na Yanga kwa penaltı 6-5 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 120 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
  Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 ni Morocco, Niger, Kongo na Eritrea ambayo imejitoa katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.
  Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Novemba 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la mshambuliaji mzaliwa wa DRC, Kokola Charles William M'Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ADOLF MTASINGWA AONGEZWA KIKOSI CHA TAIFA STARS MECHI NA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top