// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NDANDA KUCHEZA NA RUVU SHOOTING KESHO KATIKA SIKU YAO CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NDANDA KUCHEZA NA RUVU SHOOTING KESHO KATIKA SIKU YAO CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, August 19, 2017

  NDANDA KUCHEZA NA RUVU SHOOTING KESHO KATIKA SIKU YAO CHAMAZI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM 
  TIMU ya Ndanda FC itamenyana na Ruvu Shooting kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam katika tamasha la Ndanda Day, ambalo litaambatana na shamrashamra za utambulisho wa wachezaji wa kikosi cha timu hiyo msimu huu.
  Na mchezo huo utafuatia siku ya shughuli za kijamii kwa klabu hiyo, ikiwemo wachezaji pamoja na viongozi kutembelea wadi ya  wazazi kwenye hospital ya Temeke mjini Dar es Salaam.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Afisa Habari wa Ndanda FC Idrisa Bandari amesema kwamba ikiwa ni msimu wa nne wa klabu hiyo, wameona wawape nafasi wapenzi na mashabiki wa Dar es Salaam kufurahia kwa pamoja na wachezaji wao siku ya hiyo ya  Ndanda Day.
  “Tumeamua kufanya tamasha hili mjini hapa ili kuwapa nafasi  mashabiki na wapenzi wa Ndanda FC ili waweze  kuwaona  wachezaji wao. Pamoja na hilo, tutatembelea wadi ya wazazi kwenye hospitali ya Temeke, ambapo tutatoa msaada wa vitu mbalimbali,”amesema.
  Bandari amesema baada ya yote hayo, watakwenda kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaombatana na burudani kutoka kwa wasanii ambao ni wazawa wa Mtwara, ambao TID, Juma Nature, Amini, Jay Mo  na wengineo. 
  Mgeni rasmi katika siku hiyo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura na kiingilio kitakuwa Sh.2000. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDANDA KUCHEZA NA RUVU SHOOTING KESHO KATIKA SIKU YAO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top