• HABARI MPYA

    Friday, August 12, 2016

    MWANSASU ATAJA KIKOSI TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI, MAREFA NI WAGANDA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MECHI ya soka ya ufukweni kati ya Tanzania na Ivory Coast kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafiq Mugerwa katikati na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.
    Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, utarudiwa mwingine huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
    Kocha Mwansasu ametaja kikosi leo cha kuivaa Ivory Coast
    Kocha wa timu hiyo, John Mwansasu, leo Agosti 12, 2016 ametangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika Agosti 26, mwaka huu.
    Akizungumza na wandishi wa habari Mwansasu amesema kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara.
    Pia Mwansasu amesema wanatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, watarudiana huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
    Kikosi hicho kinaunda  na wachezaji Talib Ame, Ahamada, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.
    Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANSASU ATAJA KIKOSI TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI, MAREFA NI WAGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top