// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MANJI AWAONYESHA 'QIBLI' YA FEDHA MARAIS WA AFRIKA, AMWAGA MILIOMI 900 AU KWA NIABA YA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MANJI AWAONYESHA 'QIBLI' YA FEDHA MARAIS WA AFRIKA, AMWAGA MILIOMI 900 AU KWA NIABA YA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 02, 2015

    MANJI AWAONYESHA 'QIBLI' YA FEDHA MARAIS WA AFRIKA, AMWAGA MILIOMI 900 AU KWA NIABA YA YANGA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji wiki iliyopita alikuwa sehemu ya msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete uliokwenda Addis Ababa, Ethiopia kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU).  
    Na akiwa huko, milionea huyo mwenye asili ya Kiasia, ambaye bila ya  yeye kwa sasa ‘Yanga haipumui‘ ametoa msaada wa dola za Kimarekani 500,000 kiasi cha Sh. Milioni 900 za Tanzania kusaidia vita dhidi ya maradhi ya Ebola. 
    Pamoja na hayo, Manji amewasilisha pendekezo mbele ya Marais AU kuanzisha mashindano maalum ya kupambana na ugonjwa wa Ebola.
    Pendekezo hilo la Manji amelitoa Alhamisi ya Januari 29 wiki iliyopita jijini Adis Ababa nchini Ethiopia kulikofanyika mkutano huo ambao kwa nchi uliwakilishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete huku Manji akiwa mmoja wa wageni.
    Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji (kulia) amewapa dol 500,000 AU

    Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Katibu wa Yanga Dk Jonas Tibohora ambaye naye aliongozana na Manji alisema katika kikao hicho cha 24 cha AU Manji amewasilisha pendekezo hilo akitaka nchi 54 za Afrika kushiriki katika mashindano hayo mafupi kusaka fedha za kupambana na ugonjwa huo hatari unaiosumbua Afrika Magharibi kwa kuchukua washindi wawili wa juu katika kila ligi.
    Tibohora alisema katika pendekezo hilo la Manji ambalo nchi zote zililiafiki Manji ametaka mashindano hayo kuchezwa kwa kanda za nchi huzika ambapo mechi hizo zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku kila klabu ikitakiwa kuchangia kiasi cha dola 100000 (shilingi mil 170) kama kiingilio.
    Alisema lengo la Manji ni kutaka kuona soka linachangia katika mapambano ya ugonjwa huo ambapo jumla ya kiasi cha dola 10.8 ml zitaweza kupatikana huku mwenyekiti huyo akitangulia kutoa dola 500, 000 kama kianzio. 
    "Mwenyekiti amependekeza kwamba kwa kuwa Yanga tunaitwa Young African Football Club jina letu lifanye kitu kuhusu Afrika na kwa kuwa kila kanda za Afrika mfano hii ya kwetu ya Afrika Mashariki tuna utaratibu wetu wa kumaliza msimu, mashindano hayo sasa yafanyike kwa kanda ili kuweza kupatikana muda mzuri wa kuchezeka mechi hizo,"alielezea Tibohora.
    "Kwa kuwa mechi hizo zitakuwa zikiendeshwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini Manji ameomba klabu itakayocheza nyumbani itoe nusu ya mapato ya kwenye mechi husika iende katika mapambano hayo hapo pia klabu zitanufaika na nusu ya mapato hayo lakini pia ushindani huo utazinufaisha baadhi ya nchi."
    Wakati huo huo, kikosi cha Yanga kimeondoka mchana leo ikiwa na wachezaji wake wote 25 kuelekea Tanga katika mchezo wa Jumatano dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amesema hana majeruhi katika kikosi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI AWAONYESHA 'QIBLI' YA FEDHA MARAIS WA AFRIKA, AMWAGA MILIOMI 900 AU KWA NIABA YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top