Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MSAFARA wa kwanza Simba SC umeondoka jioni ya leo kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki na ushei kujiandaa na mpambano dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara huo unaojumuisha wachezaji ambao hawako timu ya taifa, Taifa Stars- umeondoka kwa ndege ya Fast Jet jioni hii ukiongozwa na kocha Mkuu, Mzambia Patrick Phiri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ambaye alikuwa Cape Town tangu juzi anatarajiwa kuupokea msafara huo Johannesburg baadaye leo.
Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani.
Wacheaji waliopo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wataondoka Dar es Salaam baada ya mechi na Benin Jumatatu.
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini kwa sababu atakuwa kwenye majukumu ya kimataifa kwao, Uganda.
Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.

![]() |
Kocha Patrick Phiri akiwa na Nahodha Msaidizi, Shaaban Kisiga 'Malone' Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati wa safari jioni ya leo |
Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani.
Wacheaji waliopo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wataondoka Dar es Salaam baada ya mechi na Benin Jumatatu.
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini kwa sababu atakuwa kwenye majukumu ya kimataifa kwao, Uganda.
Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.
![]() |
Kutoka kulia Pierre Kwizera, Meneja Nico Myagawa, Daktari Yassin Gembe na kipa Hussein Sharrif 'Cassilas' |
![]() |
Kutoka kulia Ibrahim Hajibu, Ramadhani Singano 'Messi' na William Lucian 'Gallas' |
![]() |
Msafara wa kwanza wa Simba SC umeondoka leo kwenda Afrika Kusini |
0 comments:
Post a Comment