MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba yuko fiti kuwakabili Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa Kundi G Kombe la Duani leo.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya goti lakini amesema yupo tayari kwa mchezo wa leo mjini Salvador.
"Wazi, ningeopenda kuwa fiti kwa asilimia 110- nipo fiti kwa asilimia 100 na hiyo inatosha kuisaidia timu ya taifa. Nimekuwa nikifanya mazoezi kwa siku nyingi na ninajisikia vizuri. Haujawahi kutokea wakati katika maisha yangu ya soka nikacheza bila kuwa na maumivu, huo ni mzigo,"’



.png)
0 comments:
Post a Comment