Na Mahmnoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BENDI ya Mashujaa imemnyakua rapa bora wa mwaka 2012, Kalidjo Kitokololo ‘Kuku’ kutoka FM Academia na kuingia naye Mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo katika ukumbi wa Letasi Lounge, zamani Millenium Business Park, Kijitonyama, Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi hiyo, Maximillian Luhanga amesema kwamba kumpata Chitokololo ni furaha kubwa kwao.
“Kalidjo anakuja kuwa rapa wa tatu katika bendi yetu, baada ya Saulo John maaurufu kama Ferguson na Sauti ya Radi, ambao wote ni wakali, pata picha bendi yetu itakuwa inatisha kwa kiasi gani,”amesema Luhanga.
Max amesema Kitokololo anaanza kazi mara moja baada ya kusaini mkataba mpya.
Kwa upande wake, Kitokololo mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema kwamba amekuja Tanzania kutafuta maisha na Mashujaa imempa ofa nzuri ndiyo maana amejiunga nayo.
Amesema ameondoka vizuri FM Academia akiwa amewaaga vizuri wenzake ambao wameridhia kuondoka kwake.
“Ndugu zangu wanajua mimi nimekuja Tanzania kutafuta maisha, nimewagaa na wamekubali,” amesema.
Lakini pia Kitokololo amesema kwamba amejiunga na Mashujaa kumfuata ‘baba yake wa fani’, King Dodo Labouche, Mshauri Mkuu wa bendi hiyo ambaye ndiye aliyemleta nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Mashujaa itamtambulisha rasmi mwanamuziki huyo katika onyesho maalum litakalofanyika ukumbi wa Letasi Lounge Ijumaa wiki hii.

![]() |
| Kitokololo kushoto akizungumza leo. Kulia ni Maximillian |

.png)
0 comments:
Post a Comment