Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
WAKATI kukiwa kuna kuna wasiwasi, Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage anaweza kuivunja Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Dk Damas Daniel Ndumbaro amesema hilo haliwezekani.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY katika mahojiano maalum jana mjini Dar es Salaam, Wakili Ndumbaro amesema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Simba SC, baada ya kuundwa kwa Kamati ya Uchaguzi inapaswa kufanya kazi kwa miaka miwili.
Wakili Ndumbaro amesema kwamba Kamati hiyo inaweza kuvunjwa kabla ya kufikisha muda huo, iwapo itabainika imefanya makosa na wenye uwezo wa kuivunja ni Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu.
“Rage hana uwezo wa kuivunja Kamati yetu hadi baada ya miaka miwili tangu iundwe,”amesema Ndumbaro na alipoulizwa iwapo itabainika Kamati ilifanya makosa katika utendaji wake, alijibu; “Hapo sasa ni Mkutano Mkuu ndiyo unaoweza kutuondoa sisi hapa,”.
Ndumbaro alipoulizwa kama TFF kupitia Kamati zake zina uwezo wa kuivunja Kamati hiyo, alijibu; “Haiwezi,”.
Alipoulizwa nini hatima ya mustakabali wa klabu ya Simba SC kwa sasa, kufuatia mgogoro wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu ambao umesimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ndumbaro alisema; “FIFA, FIFA ndiyo itaamua”.
Ndumbaro amesema kwamba “Duniani kote Kamati za Uchaguzi huwa ni huru, haziingiliwi, sisi tuna bahati sana tuna kanuni. Kamati ikifanya maamuzi imefanya. Mbele ya macho ya sheria maamuzi ya TFF ni batili,”.
Ikumbukwe chanzo cha mgogoro huu ni Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua mgombea Urais Michael Richard Wambura kwa sababu alikiuka Katiba kwa kuipeleka klabu hiyo Mahakamani, jambo ambalo FIFA inakataza.
Wambura alikata rufaa, Kamati ya Rufani ya TFF chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya, ambako alishinda na kurejeshwa kwenye kinyang’anyiro. Wakili Lugaziya alisema Kamati yake iliamua kumrejesha Wambura kwa sababu baada ya kosa alilolifanya aliendelea kuhudhuria mikutano ya klabu, kulipia ada zake za uanachama na pia akateuliwa katika Kamati ya Utendaji, iliyounda Kamati ya Uchaguzi ya sasa chini ya Ndumbaro.
Hata hivyo, Jumapili Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema ameusimamisha uchaguzi wa Simba SC kwanza hadi uongozi wa klabu hiyo uunde Kamati ya Maadili ambayo itashughulikia kesi za kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Ndumbaro amepinga hilo, akisema TFF haiwezi kusimamisha Uchaguzi wa Simba SC na pia amesema hawezi kumpokea Wambura katika uchaguzi, kwa sababu mgombea huyo alishiriki shughuli za klabu kimakosa baada ya kukiuka Katiba kwa kwenda Mahakamani.
“Ubatili haupaswi kufumbiwa macho, hakuna kosa linalohalalisha kosa, kama mtu alifanya kosa, watu wakajisahau kidogo, haimaanishi imefuta kosa la nyuma,”alisema.
Dk Ndumbaro amesema kwamba kwa sasa hatima ya uchaguzi wa Simba SC ni FIFA kuingilia na wapo wapo tayari kulipeleka suala hilo huko.

![]() |
| Hawezi ng'o; Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC, Wakili Dk Damas Ndumbaro amesema Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Rage hawezi kuivunja Kamati hiyo |

.png)
0 comments:
Post a Comment