Na Samira Said, DAR ES SALAAM
WANACHAMA wa Simba SC mchana wa leo wakiwa wameshika kadi zao mkononi walifika makao makuu ya klabu hiyo wakisema kuwa wanataka uchaguzi uendelee.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa niaba ya wanachama wenzake, Ras Simba (05757), amesema kuwa maamuzi ya Malinzi ni ya kukurupuka na wao wanataka zoezi la uchaguzi liendelee.
Simba alisema kwamba kitendo cha kuusimamisha uchaguzi huo ni kuiingilia klabu hiyo kuelekea kipindi muhimu cha usajili na maandalizi ya timu.
"Maamuzi yake mengi ni ya kukurupuka, hata alipomtaka Rage (Ismail) aitishe mkutano mkuu, alimgomea, hata sisi hatutaki asituingilie," alisema mwanachama huyo.
Fihi Kambi (04717), alisema kuwa kwa nini kiongozi huyo amesimamisha uchaguzi baada ya Kamati ya Maadili kutakiwa kukutana, na akahoji ameona nini kitafuata.
Paul Makoye (537) alisema kuwa alimtaka Malinzi awe mwaminifu kwa katiba ya TFF na wanachama wa shirikisho hilo.
Naye Ustadh Masoud alisema kuwa anataka kuona mchakato wa uchaguzi unaendelea kama ulivyotangazwa na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo.
Mwanachama huyo mwenye kadi namba 536 kutoka Mpira Pesa alisema kuwa pia malalamiko yake ya kimaadili dhidi ya Michael Wambura, anajipanga kuyapeleka FIFA ili yakasikilizwe.
Alisema kuwa amefikia maamuzi hayo kufuatia kauli ya TFF kusitisha Kamati yake ya Maadili kusikiliza malalamiko yake na ya wanachama wengine wa Simba.
WANACHAMA wa Simba SC mchana wa leo wakiwa wameshika kadi zao mkononi walifika makao makuu ya klabu hiyo wakisema kuwa wanataka uchaguzi uendelee.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa niaba ya wanachama wenzake, Ras Simba (05757), amesema kuwa maamuzi ya Malinzi ni ya kukurupuka na wao wanataka zoezi la uchaguzi liendelee.
![]() |
| Ras Simba akizungumza na Waandishi wa Habari leo Msimbazi |
"Maamuzi yake mengi ni ya kukurupuka, hata alipomtaka Rage (Ismail) aitishe mkutano mkuu, alimgomea, hata sisi hatutaki asituingilie," alisema mwanachama huyo.
Fihi Kambi (04717), alisema kuwa kwa nini kiongozi huyo amesimamisha uchaguzi baada ya Kamati ya Maadili kutakiwa kukutana, na akahoji ameona nini kitafuata.
Paul Makoye (537) alisema kuwa alimtaka Malinzi awe mwaminifu kwa katiba ya TFF na wanachama wa shirikisho hilo.
Naye Ustadh Masoud alisema kuwa anataka kuona mchakato wa uchaguzi unaendelea kama ulivyotangazwa na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo.
Mwanachama huyo mwenye kadi namba 536 kutoka Mpira Pesa alisema kuwa pia malalamiko yake ya kimaadili dhidi ya Michael Wambura, anajipanga kuyapeleka FIFA ili yakasikilizwe.
Alisema kuwa amefikia maamuzi hayo kufuatia kauli ya TFF kusitisha Kamati yake ya Maadili kusikiliza malalamiko yake na ya wanachama wengine wa Simba.

.png)
0 comments:
Post a Comment