• HABARI MPYA

    Monday, June 16, 2014

    FIGO, HIERO WATAMANI HATA KESHO WAJE TANZANIA, YATHIBITISHWA BECKHAM, RONALDO LIMA, RAUL NA ROBERTO CARLOS PIA WATAKUJA NA REAL MADRID AGOSTI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MAGWIJI wa Real Madrid ya Hispania, Fernando Hiero na Luis Figo wamekaririwa wakisema kwamba wanatamani Agosti ifike kesho ili waweze kuja Tanzania, imeelezwa.  
    Mkurugenzi wa makampuni ya TSN, Farouqh Baghozah ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu leo kutoka Brazil kwamba, amekutana na Figo leo mjini Rio de Jeneiro nchini humo kwenye Kombe la Dunia na kuzungumzia ziara yao ya Agosti nchini.
    Kikosi cha magwiji waliowika Real Madrid kuanzia muongo uliopita, kitazuru nchini Agosti na kucheza mechi ya kirafiki pamoja na kufanya utalii katika vivutio mbalimbali nchini kwa mwaliko wa makampuni ya TSN.
    Tunakuja; Luis Figo kulia na Fernando Hiero kushoto wamesema wanatamani Agosti ifike kesho waje Tanzania 

    Na Baghozah ambaye kwa sasa yupo Brazil kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia, amesema; “Nimekutana na Fernando Hiero na Figo, kwa kweli wamevutiwa sana na ziara hii, yaani wanatamani hiyo siku ifike kesho waje,”.
    TFF, Shirikisho la Soka Tanzania imehusishwa katika ziara hiyo na imesema itateua kikosi maalum cha nyota wa Tanzania kucheza na wachezaji hao waliotamba Real enzi hizo wakiitwa Magalactico. 
    “Nimekuwa na hawa jamaa tangu Ureno kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya hapo wakanialika Madrid, kwa kweli wana hamu sana na ziara hii,”amesema Baghozah.

    Wachezaji 11 waliokuwa wakiunda Real Madrid ya Magalacticos II kuanzia mwaka 1997 hadi 2003, Roberto Carlos, Fernando Hierro, Fernando Redondo, Luis Figo, Zinedine Zidane na Raul Gonzalez ambao katika kipindi hicho walishinda mataji mawili ya La Liga, matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya Kombe la Mabara na moja la League Standard.

    Mkurugenzi huyo wa makampuni ya TSN, amesema wamemthibitishia wachezaji wote nyota waliowika Real muongo uliopita wakiwemo Zinadine Zidane, David Beckham, Figo, Roberto Carlos, Ronaldo Lima na Raul Gonzalez watakuja nchini.
    “Nawasiliana na wenzangu nyumbani (Tanzania), kwa ujumla maandalizi ya ziara hiyo yanaendelea vizuri na ni tumaini langu litakuwa tukio moja kubwa sana na la kihistoria,”amesema Baghozah.     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIGO, HIERO WATAMANI HATA KESHO WAJE TANZANIA, YATHIBITISHWA BECKHAM, RONALDO LIMA, RAUL NA ROBERTO CARLOS PIA WATAKUJA NA REAL MADRID AGOSTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top