// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BIN SLUM WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI MBEYA CITY, COASTAL UNION WATAJIJUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BIN SLUM WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI MBEYA CITY, COASTAL UNION WATAJIJUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 05, 2014

    BIN SLUM WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI MBEYA CITY, COASTAL UNION WATAJIJUU

    Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI Bin Slum Tyres Limited, imeingia mkataba wa udhamini na klabu ya Mbeya City FC ya Mbeya wa miaka miwili wenye thamani ya Sh. Milioni 360.
    Katika Mkataba huo, uliosainiwa leo makao makuu ya Bin Slum Tyres mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, Mbeya City watavaa jezi zenye nembo ya RB Battery, moja ya bidhaa zinaouzwa na kampuni hiyo.  
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bin Slum Tyres Limited, Nassor Bin Slum amesema kwamba sababu kubwa tatu zimewasukuma kuwekeza katika klabu hiyo.
    Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres Limited, Mohammed Bin Slum kulia akitiliana saini mikataba na Mwanasheria wa Mbeya City kushoto leo mjini Dar es Salaam

    Amezitaja sababu hizo kuwa ni kuuzika kwa wingi kwa bidhaa za kampuni yake kwa sasa katika Jiji la Mbeya, kuvutiwa na uongozi bora wa klabu hiyo na tatu kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
    “Kwa sasa mkoa wa Mbeya ni ambao nina wateja wengi wa bidhaa zangu, kwa hiyo hilo ni la kwanza limenivutia kuwekeza katika klabu hiyo.
    Pili, uongozi. Hii timu ina uongozi bora wenye sera nzuri na uwajibikaji bora, ambao umeifanya Mbeya City iwe maarufu nchini ndani ya muda mfupi tu tangu ipande Ligi Kuu.
    Tatu, Mheshimiwa Rais wetu Jakaya Kikwete alishauri makampuni yawekeze katika timu za mikoani ili kuzijengea uwezo nazo pia, badala ya kusaidia timu kubwa pekee Simba na Yanga ambazo tayari zina vyanzo vingi vya mapato,”amesema Bin Slum.
    Kwa miaka kadhaa Bin Slum Tyres limited imekuwa ikiidhamini klabu ya Coastal Union ya Tanga, lakini mwishoni mwa msimu huu iliingia katika mgogoro na uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Ally Hemed ‘Aurora’.
    Wazi kujitoa kwa Bin Slum Tyres Limited katika klabu ya Coastal ni pigo kubwa, kwa sababu kampuni hiyo imekuwa ikijitolea kwa hali na mali kuisaidia klabu hiyo- mapenzi binafasi ya wenye kampuni hiyo na klabu hiyo yakichangia.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BIN SLUM WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI MBEYA CITY, COASTAL UNION WATAJIJUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top