Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
WAKATI kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi anatamba kuiharibia Azam FC Jumapili, timu hiyo ya Wanalambalamba itakuwa na mtihani mgumu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ambao wenyeji hawajapoteza hata mechi moja msimu huu.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu jana mchana akiwa jijini Mbeya, Mwambusi amesema vijana wake wako kamili kuiua Azam katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 3-3 mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam Novemba 7, mwaka jana.
MZUNGUKO WA KWANZA
SOKOINE
Mbeya City 0-0 Kagera (Agosti 24, 2013)
Mbeya City 2-1 Ruvu (Agosti 28, 2013)
Mbeya City 1-1 Yanga (Sept 14, 2013)
Mbeya City 1-1 Coastal (Sept 28, 2013)
Mbeya City 1-0 JKT (Okt 19, 2013)
Prisons 0-2 Mbeya City (Okt 29, 2013)
Mbeya City 1-0 Ashanti (Nov 2, 2013)
UGENINI
Mtibwa 0-0 Mbeya City (Sept 18, 2013)
Simba 2-2 Mbeya City (Sept 21, 2013)
Oljoro 1-2 Mbeya City (Okt 5, 2013)
Rhino 1-3 Mbeya City (Okt 9, 2013)
Mgambo 0-1 Mbeya City (Okt 13, 2013)
Mbeya City 3-3 Azam (Novemba 7, 2013)
MZUNGUKO WA PILI
SOKOINE
Mbeya City 2-1 Mtibwa (Feb 9, 2014)
Mbeya City 1-1 Simba (Feb 15, 2014)
Mbeya City 0-0 Oljoro (Machi 3, 2014)
Mbeya City 3-0 Rhino (Machi 8, 2014)
Mbeya City 1-0 Prisons (Machi 30, 2014)
UGENINI
Kagera 0-1 Mbeya City (Jan 25, 2014)
Ruvu 1-1 Mbeya City (Jan 29, 2014)
Yanga 1-0 Mbeya City (Feb 2, 2014)
Coastal 2-0 Mbeya City (Feb 22, 2014)
JKT 1-2 Mbeya City Machi 22, 2014)
Ashanti 0-0 Mbeya City (Apr 5, 2014)
"Tunatambua Azam hawajapoteza mechi, lakini lazima wajue tunahitaji kulinda heshima pia ya kutofungwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani msimu huu. Tutambana hadi dakika ya mwisho ili tushinde mechi hiyo," amesema Mwambusi.
Mbeya City imecheza mechi 12 kwenye Uwanja huo ikishinda nne na sare tatu mzunguko wa kwanza, huku mzunguko wa pili ikishinda tatu na kutoka sare mara mbili.
Lakini, Azam FC hawajapoteza hata mechi moja msimu huu huku wakiweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga dhidi ya Mgambo JKT mzunguko wa pili wakati Yanga na Simba wamechezea kichapo kwenye uwanja huo dhidi ya timu hiyo inayopigana kuukwepa mstari wa kuporomoka daraja.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kalimangonga Ongala 'Kally' alisema jana: "Baada ya ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, tunaelekeza nguvu zetu kwa Mbeya City ambayo pia ni timu nzuri na tunapaswa kujipanga zaidi kabla ya kuvaana nayo."
Azam FC inaondoka leo asubuhi kwa ndege kuifuata Mbeya City baada ya Alhamisi kuifunga Ruvu Shooting mabao 3-0 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Azam FC inashikilia usukani wa ligi ikiwa na pointi 56, nne mbele ya Yanga waliopo nafasi ya pili wakati Mbeya City iliyoshinda mechi 12, sare 10 na kupoteza mbili msimu huu inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46.

![]() |
Kocha Juma Mwambusi wa Mbeya City amesema kwamba wanataka kulinda heshima ya kutofungwa Uwanja wa Sokoine TAKWIMU ZA MBEYA CITY |

0 comments:
Post a Comment