• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2016

  YANGA WAFUATA POINTI SITA SHINYANGA LEO...MWADUI NA STAND WAJIPANGE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi, Yanga SC wanaaondoka Alfajiri ya leo kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mwadui.
  Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm wiki alihamishia mazoezi ya timu yake kwenye Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam kwa sababu ‘ni mbovu mbovu’ kama Kambarage.
  Kwa sasa Uwanja maarufu wa mazoezi wa Yanga ni Gymkhana, Dar es Salaam lakini kuelekea mechi za Kanda ya Ziwa, Pluijm alipeleka timu Kaunda.
  Kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kwenda Shinyanga ni Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Benno Kakolanya na Deo Munishi ‘Dida’, mabeki; Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’ na Pato Ngonyani. 
  Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Geoffrey Mwashiuya, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Yussuf Mhilu, Juma Mahadhi na washambuliaji Matheo Anthony, Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
  Na kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea wikiendi hii, mbali ya Yanga na kuwa wageni wa Mwadui, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Azam FC watamenyana na Simba SC na Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Mtibwa Sugar na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Ruvu Shooting na Mbao FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Maji Maji na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
  Jumapili kutakuwa na michezo miwili, Stand United wakiikaribisha JKT Ruvu Stars Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na African Lyon wakimenyana na Toto Africans Uwanja wa Uhuru.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAFUATA POINTI SITA SHINYANGA LEO...MWADUI NA STAND WAJIPANGE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top