• HABARI MPYA

    Wednesday, September 07, 2016

    TEMEKE YAANZA NA MOTO AIRTEL RISING STARS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    PAZIA la michuano Taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jana lilifunguliwa katika uwanja wa Kukumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ambapo timu ya wavulana ya Temeke ilitoa onyo kali kwa timu shiriki kwa kuifunga Kinondoni 4-1.
    Mchezo huo ulitanguliwa na mechi ya wasichana kati ya Arusha na Lindi ambapo Arusha waliibuka na ushindi wa 2-0. Magoli ya Arusha yalifungwa na Eva Michael dakika ya 39 kwa njia ya penalti na pili likifungwa na Warda Alfonce dakika ya 60.
    Mchezaji wa Arusha, Diana Mosses (kulia) akiwania mpira na beki wa Lindi , Neema Hashim katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana

    Katika mchezo wa Temeke na Kinondoni, Temeke walianza kwa kasi ya aina yake na kupeleka mashambuliazi ya mara kwa mara langoni mwa Kinondoni huku Kinondoni wakionekana kuzidiwa katika kila idara.
    Temeke waliandika bao la kwanza kupitia kwa Ramadhan Kawambwa kaika dakika ya 14, kwa njia ya penati baada ya mchezaji wa Temeke kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari. Goli hilo lilipokelewa kwa shangwa na mashabiki wa Temeke.
    Temeke awalipata bao lao la pili kupitia kwa Abirahi Uihuro mnamo dakika ya 34 ambaye aligongeana mpira kwa uzuri na Ismail Kovu na kisha kumchambua kipa wa Kinondoni kwa umaridadi wa hali ya juu na kuukwamisha mpira huo kimiani.
    Mohammed Mbegu aliifungia Temeke bao la tatu katika dakika ya 40 na kuzidi kuzamisha jahazi la Kinondoni ambao walinekana kama vile wamesimama wakati mchezo ukiendelea.
    Rosea Mpoma aliwaliza kwa mara nyingine tena Arusha baada ya kuifungia Temeke bao la tano katika dakika ya 53 baada ya kuachia shuti kali na kuzama moja kwa moja wavuni.
    Alikuwa ni Abirahi Uihuro tena, ambaye aliiandikia Temeka bao la nne mnamo dakika ya 28 ya kipindi cha pili baada ya kuunganisha krosi iliyochongwa na Mohammed Mbegu kutoka upande wa kushoto mwa uwanja na kuendeleza karamu ya magoli kwa Temeke.
    Kinondoni walipata goli ya kufuta machozi mnamo dakika 36, likifungwa na Shaban Mangula baada ya mabeki ya Temeke kushindwa kuokoa mpira wa kona.
    Michuano hiyo ya Airtel Rising Stars itaendelea kesho kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kufikia tamati Jumapili, Septemba 11.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEMEKE YAANZA NA MOTO AIRTEL RISING STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top