• HABARI MPYA

  Tuesday, February 02, 2016

  MAZEMBE YAINGIA KWENYE MJADALA WA KUWANUNUA CHANONGO, UBWA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KLABU ya TP Mazembe ya DRC imeingia katika mazungumzo ya kuwanunua wachezaji wawili wa Stand United, beki Abuu Ubwa na kiungo Haroun Chanongo baada ya kufanya vizuri katika majaribio yao mapema Januari.
  Wawili hao walisafiri hadi Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mapema Januari kwa majaribio ya wiki moja na taarifa za awali zikasema, wamefuzu.
  Meneja wa wachezaji hao, Jamal Kisongo amesema tayari Mazembe imetuma barua rasmi ya majibu ya majaribio ya vijana hao na kwamba sasa wanaingia katika mazungumzo na klabu yake.
  Abuu Ubwa (kulia) na Haroun Chanongo (kushoto) wako mbioni kujiunga na TP Mazembe

  “Jana nimepokea taarifa rasmi kutoka Mazembe kwamba (Chanongo na Ubwa) wamefuzu. Tunatarajia watasaini Mkataba wakati wowote baada ya kukamilika kwa mazungumzo na klabu yao,”amesema Kisongo akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo.
  Kisongo ambaye pia ni Meneja wa mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba mazungumzo rasmi yatafanyika baada ya Rais wa Mazembe, Moise Katumbi kurejea Lubumbashi kutoka Ulaya.
  Baada ya kuonja matunda ya washambuliaji wawili wa Kitanzania, Samatta kabla ya kuhamia Genk mwishoni mwa mwezi uliopita na Thomas Ulimwengu ambao kwa pamoja wamekuwa Lubumbashi kwa miaka mine wakitoa huduma, Mazembe sasa imefungua milango zaidi kwa wachezaji wa Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YAINGIA KWENYE MJADALA WA KUWANUNUA CHANONGO, UBWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top