• HABARI MPYA

    Monday, February 01, 2016

    KAVUMBANGU ANUSURIKA KIFO CHA AJALI DAR, GARI YAKE ‘NYANG’ANYANG’A’

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu, anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, leo amenusurika katika ajali mbaya, lakini gari yake aina ya Toyota Premio  ‘halitamaniki’.
    Kavumbangu ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati anatoka nyumbani kwake, Kijichi kwenda hospitali ya Dk Gilbert, Mikocheni kwa matibabu ya majeruhi yake yanayomuweka nje tangu mwezi uliopita.
    Gari ya Didier Kabumbangu (picha ndogo kulia) inavyoonekana kwa mbele baada ya ajali
    Mipira ya kumzuia aliye ndani ya gari asiumie ikiwa imechomoka kutokana na ajali hiyo 

    Amesema wakati anakata kona kwenye mzunguko wa magari yanayotoka Kijichi na Mbagala kuelekea mjini, ndipo alipogongwa na gari kubwa la mizigo, ambalo ‘limeiharibu sura’ gari yake kwa mbele.
    “Kisheria inatakiwa wale wanaotoka Mbagala watusubiri sisi tunaozunguka tupite, lakini jamaa hakusimama akapita na moto akaipitia gari yangu kwa mbele yote imeharibika sura,”amesema.
    Didier Kavumbangu amekuwa nje tangu mwezi uliopita kutokana na majeruhi

    Na Kavumbangu anasikitika jamaa baada ya kugonga hakusimama akakimbia na hakukuwa na trafiki karibu wa kuja japo kupima ajali.
    “Kwa kuwa mimi sikuumia, nikaona hapa nitapoteza muda bure, nikaita gari la kuvuta gari yangu, mimi nikaenda zangu kwa Dokta Gilbert,”amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
    Toyota Premio ya Kavumbangu inavyoonekana kikamilifu baada ya ajali leo


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAVUMBANGU ANUSURIKA KIFO CHA AJALI DAR, GARI YAKE ‘NYANG’ANYANG’A’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top