• HABARI MPYA

  Tuesday, February 16, 2016

  BEKI YANGA SC AICHAMBUA FOWADI SIMBA SC, ASEMA; "KIIZA NA HAJIB BALAA TUPU"

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ULIKUWA hujui nani mkali kati ya washambuliaji wawili wa Simba SC, Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ na mtoto wa nyumbani, Ibrahim Hajib? Basi beki wa zamani wa Yanga SC, Ibrahim Job ana majibu leo.
  Mlinzi huyo mrefu na mkabaji mzuri, amesema Hajib anazidi ubora straika mwenzake, Hamisi Kiiza na kwamba pia hao ni washambuliaji wawili wa aina tofauti.
  Job ambaye kwa sasa anacheza Kagera Sugar amesema; “Ni vigumu kwa beki kucheza dhidi ya Hajib na si Kiiza. Hajib ana kipaji na anajua kuuchezea mpira kwenye mazingira ambayo anakuwa akipambana na beki mmoja,”.
  Fowadi hatari; Hamisi Kiiza (kulia) na Ibrahim Hajib (kushoto)

  “Kiiza nimecheza naye Yanga kwa zaidi ya miaka miwili, lakini yeye ni mfungaji tu, hayuko vizuri kama alivyo Hajib kwenye kuuchezea mpira, dogo huyo ni habari nyingine.
  “Makocha wetu pia wamekuwa wakituelekeza zaidi jinsi ya kumdhibiti Hajib na si Kiiza, kitu ambacho kinadhihirisha kwamba Hajib ni hatari na anaweza kufanya chochote anapokuwa na mpira, tena akiwa karibu na lango la timu pinzani,” alisema.
  Beki huyo aliyewahi pia kuchezea Toto African na African Lyon, amesema kwamba Hajib ni moja ya washambuliaji wagumu kuwadhibiti kutokana na kipaji alichonacho cha kuuchezea mpira, lakini pia akadai kuwa winga wa Azam, Ramadhani Singano ‘Messi’ ni mchezaji mwingine aliyekuwa ‘akimpa taabu’ miaka ya nyuma. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI YANGA SC AICHAMBUA FOWADI SIMBA SC, ASEMA; "KIIZA NA HAJIB BALAA TUPU" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top