• HABARI MPYA

  Wednesday, February 17, 2016

  AZAM TV NA TIGO PESA KUPELEKA WAWILI HISPANIA KUISHUHUDIA BARCA LA LIGA

  Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam TV, Mgope Kiwanga (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Azam TV, Tabata, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya kujishindia safari ya kwenda kushuhudiamechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu. Kushoto ni Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta. 
  Naibu Mkurugenzi wa Azam TV, Tido Mhando akifuatilia mkutano huo leo Tabata.

  Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington (kushoto) akizungumza. Promotion hiyo ya ushirikiano wa Tigo Pesa na Azam TV, inaanza rasmi leo hadi Machi 13 na washindi wawili watakwenda Hispania.

  Wenye Azam TV yao; Kutoka kulia ni Yahya Mohammed, Baruwani Muhuza, Tido Mhando na Charles Hillary waakifuatilia uzinduzi wa promosheni hiyo. Ili kushiriki, unatakiwa kulipia kifurushi cha Azam Sports HD kwa miezi miwili kwa bei ya punguzo, Sh 22,000 kupitia Tigo Pesa na utaingia kwenye droo, ambayo washindi wengine 10 watapata zawadi mbalimbali kila wiki zikiwemo jezi za kiwango cha juu cha ubora, fulana za La Liga, mpira wa ubora wa hali ya juu, peni, cha kushikia funguo, miwani ya La Liga Na nyinginezo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM TV NA TIGO PESA KUPELEKA WAWILI HISPANIA KUISHUHUDIA BARCA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top