• HABARI MPYA

    Monday, November 22, 2021

    YANGA SC YAKUBALI YAISHE KWA MORRISON


    KLABU ya Yanga imekubaliana na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kutupilia mbali kesi yao dhidi ya winga Mghana, Bernard Morrison.
    “Matokeo ya kesi hii hayatoirudisha nyuma klabu ya Yanga katika kupambania haki zake pale itakapoona inafaa kufanya hivyo,”imesema taarifa ya Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla.
    Mapema leo taarifa ya CAS ilisema kwamba mkataba wa awali wa Yanga na Morrison ulimalizika Julai 14, mwaka 2020 na wa pili ambao Mghana huyo anaukana alisharejesha fedha za klabu hiyo dola za Kimarekani 30,000 hivyo hakuna kesi baina yao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAKUBALI YAISHE KWA MORRISON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top