• HABARI MPYA

  Sunday, November 21, 2021

  KMC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU


  TIMU ya KMC imepata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuichapa Azam FC 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC leo yamefungwa na Matheo Anthony Simon dakika ya 13 na Hassan Salum Kabunda dakika ya 90, huku la Azam FC likifungwa na Mzambia, Charles Zullu dakika ya 43.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi tano na kupanda kwa nafasi mbili kutoka mkiani katika ligi ya timu ya timu 16.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Anuary Jabir alianza kuifungia Dodoma Jiji dakika ya 10, kabla ya Deogratius Mafie kuisawazishia Biashara United dakika ya 63.
  Dodoma Jiji inafikisha pointi 11, ingawa inabaki nafasi ya tatu na Biashara inafikisha pointi saba na inaendelea kushika nafasi ya saba baada ya timu zote kucheza mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top