• HABARI MPYA

  Tuesday, November 09, 2021

  TANZANITE YAIBUGIZA DJIBOUTI 8-0 UGANDA


  TANZANIA 
  imemalizia hasira zake kwa Djibouti kwa kuitandika 8-0 katika mechi yake ya mwisho ya michuano ya  CECAFA wanawake U20 Uwanja wa FTC Njeru nchini Uganda.
  Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Aisha Masaka saba dakika ya tatu, 27, 60, 66, 72, 73 na 86  na lingine Clara Luvanga dakika ya 43.
  Mechi nne za awaliTanzanite ilishinda mbili 1-0 dhidi ya Eritrea na 3-2 dhidi ya Burundi na pia ilifungwa mbili, 1-0 na wenyeji, Uganda na 2-1 na Ethiopia.
  Kwa matokeo hayo, Tanzanite inamaliza nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa, Uganda na Ethiopia.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YAIBUGIZA DJIBOUTI 8-0 UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top