• HABARI MPYA

  Thursday, November 11, 2021

  TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 NA DRC DAR

  TANZANIA imepoteza nafasi ya kufuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuchapwa 3-0 nyumbani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Leopards yamefungwa na kiungo wa Lille ya Ufaransa, Gael Romeo Kakuta Mambenga dakika ya sita, beki wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Idumba Fasika na mshambuliaji wa Sharjah ya Dubai, Ben Malango Ngita dakika ya 85.
  Kwa matokeo hayo, Leopards inafikisha pointi nane na kupanda nafasi ya pili Kundi J ikiizidi pointi moja Taifa Stars kuelekea mechi za mwisho Jumapili.


  Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya 
  Madagascar Uwanja wa l'Amitié Jijini CotonouBenin sasa inangoza kundi hilo kwa pointi zake 10 kuelekea mechi ya mwisho na DRC Jumapili Kinshasa.
  Madagascar watakuwa wenyeji wa Tanzania kwenye mechi ya mwisho Jumapili Jijini Antananarivo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 NA DRC DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top