• HABARI MPYA

  Friday, November 19, 2021

  TANZANIA YATOA MCHEZAJI BORA COSAFA


  MTANZANIA Erick Manyama amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi ya Kundi B michuano ya COSAFA Soka la Ufukweni akiiwezesha timu yake ya taifa kushinda 2-1 dhidi ya Comoro Alhamisi Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Tanzania imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya kufanya vizuri katika mechi zake mbili za Alhamisi ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Comoro, Tanzania ilifungwa kwa penalti 4-3 na Msumbiji kufuatia sare ya 4-4 South Beach Arena.
  Sasa Tanzania itamenyana na Angola katika mechi ya Nusu Fainali Ijumaa hapo hapo South Beach Arena, wakati Msumbiji itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini katika Nusu Fainali nyingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATOA MCHEZAJI BORA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top