• HABARI MPYA

  Friday, November 19, 2021

  TANZANIA YATINGA FAINALI COSAFA UFUKWENI


  TANZANIA imefanikiwa kuingia fainali michuano ya COSAFA Soka la Ufukweni baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Angola leo ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban, Afrika Kusini. 


  Mchezaji wa Tanzania, Stephano Manyama amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na sasa timu hiyo ya kocha Boniphace Pawasa itakutana na Msumbiji katika fainali Jumapili. 


  Msumbiji ambayo iliifunga Tanzania kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4 katika mchezo wa Kundi B jana, leo imewafunga wenyeji, Afrika Kusini 5-3 katika Nusu Fainali nyingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATINGA FAINALI COSAFA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top