• HABARI MPYA

    Tuesday, November 16, 2021

    YANGA ILISHINDA KURA SHEREHE ZA RAIS MWINYI

    KLABU ya Yanga ilichaguliwa kwa kura nyingi zaidi kushiriki sherehe za mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.
    Wizara ya Habari Utamaduni Vijana Sanaa na Michezo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, SMZ leo  imesema walikuwa na mapendekezo ya timu tatu katika kufanikisha sherehe hizo ambazo ni kutoka bara yaani Azam, Simba na Yanga na ndipo kura zikawapatia mwalilwa.
    Katibu mkuu wizara hiyo Bi Fatma Hamad Rajab amesema Leo visiwani humo katika kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe hizo ambazo zilifana.
    "Tulipeleka timu tatu kwa wadau ili zipigiwe kura ni timu ipi tuialike kuja kusheherehesha ambazo kutoka bara tulipendekeza Yanga, Simba na Azam na baada ya mchakato wa kama wiki hivi timu pekee iliyopata kura nyingi ni Yanga. hivyo tulipeleka mwaliko na tukawaambia kabisa viongozi wa Yanga, wadau wenu visiwani wanahitaji mje kutoa burudani," amesema Fatma.
    Katika kura zaidi ya 5500 zilizopigwa na wadau wa soka hapa visiwani YANGA ilipata kura 4915, Simba ilipata kura 422 na Azam ilipata kura 163 pekee--bi FATMA HAMAD RAJAB
    Hatukuwa na namna zaidi ya kuwasiliana na uongozi wa YANGA ambao nao walitupa ushirikiano mkubwa na kuahidi kuleta kikosi Chao kamili Ili kutoa burudani kwa wapenda soka hapa visiwani na kama mlivyoona wenyewe Yanga waliuwasha hasa hivyo tunawashukuru hawakutuangusha--bi FATMA
    Imani ya wazanzibar kwa timu za bara hasa YANGA ni kubwa mno hivyo kwa kutambua Hilo viongozi wa YANGA nao waliitikia mualiko wetu vizuri na hawakutaka kuleta kikosi B kwani walituambia wachezaji pekee watakaokosekana ni wale tu walioitwa kwenye timu zao za taifa lakini wengine wote watakuja nao na walifanya hivyo sisi kama wizara na ambao tulipewa jukumu la kuratibu Hilo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa YANGA na mashabiki kwa ujumla--alimalizia bi FATMA HAMAD RAJAB
    Katibu mkuu wizara hiyo Bi Fatma Hamad Rajab amesema Leo visiwani humo katika kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe hizo ambazo zilifana.
    "Tulipeleka timu tatu kwa wadau ili zipigiwe kura ni timu ipi tuialike kuja kusheherehesha ambazo kutoka bara tulipendekeza Yanga, Simba na Azam na baada ya mchakato wa kama wiki hivi timu pekee iliyopata kura nyingi ni Yanga. hivyo tulipeleka mwaliko na tukawaambia kabisa viongozi wa Yanga, wadau wenu visiwani wanahitaji mje kutoa burudani," amesema Fatma.
    Katika kura zaidi ya 5500 zilizopigwa na wadau wa soka hapa visiwani YANGA ilipata kura 4915, Simba ilipata kura 422 na Azam ilipata kura 163 pekee--bi FATMA HAMAD RAJAB.
    Hatukuwa na namna zaidi ya kuwasiliana na uongozi wa YANGA ambao nao walitupa ushirikiano mkubwa na kuahidi kuleta kikosi Chao kamili Ili kutoa burudani kwa wapenda soka hapa visiwani na kama mlivyoona wenyewe Yanga waliuwasha hasa hivyo tunawashukuru hawakutuangusha--bi FATMA.
    Imani ya wazanzibar kwa timu za bara hasa YANGA ni kubwa mno hivyo kwa kutambua Hilo viongozi wa YANGA nao waliitikia mualiko wetu vizuri na hawakutaka kuleta kikosi B kwani walituambia wachezaji pekee watakaokosekana ni wale tu walioitwa kwenye timu zao za taifa lakini wengine wote watakuja nao na walifanya hivyo sisi kama wizara na ambao tulipewa jukumu la kuratibu Hilo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa YANGA na mashabiki kwa ujumla--alimalizia bi FATMA HAMAD RAJAB
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA ILISHINDA KURA SHEREHE ZA RAIS MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top