• HABARI MPYA

  Tuesday, November 09, 2021

  YANGA SC YAICHAPA MLANDEGE 1-0 ZENJI


  BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Heritier Ebenezer Makambo dakika ya 50 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mlandege FC katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 
  Yanga iliwasili Zanzibar mapema leo kuweka kambi ya wiki moja na ushei kujiandaa na mechi yake ijayo Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Namungo FC Novemba 20 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
  Baada ya mchezo wa leo, Yanga iitateremka tena dimbani Novemba 12 kumenyana na  KMKM hapo hapo Amaan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA MLANDEGE 1-0 ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top