• HABARI MPYA

  Tuesday, November 02, 2021

  YANGA YATOKA NYUMA KUSHINDA 3-1


  VIGOGO, Yanga SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ruvu Shooting walitangulia kwa bao la Shaaban Msala dakika ya tisa akimalizia pasi ya Nathaniel Chilambo, kabla ya Yanga kupambana na kupindua meza.
  Kiungo Feisal Salum alianza kuisawazishia Yanga dakika ya 32, kabla ya Wakongo, beki Djuma Shabani kufunga la pili dakika ya 48 kwa penalti na kiungo Mukoko Tonombe kufunga la tatu dakika ya 75 akimalizia kazi nzuri ya kiungo mzawa, Farid Mussa.
  Ruvu Shooting inayofundishwa na kocha mzawa, Charles Boniface Mkwasa ilimaliza pungufu baada y mchezaji wake, Santos Mazengo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 24.
  Yanga inafikisha pointi 15 baada ya kushinda mechi zote tano tangu msimu uanze na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya Polisi Tanzania wanaofuatia wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake sita za mechi tano sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YATOKA NYUMA KUSHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top