• HABARI MPYA

  Thursday, November 18, 2021

  TANZANIA YATINGA NUSU FAINALI COSAFA UFUKWENI


  TANZANIA imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Soka la Ufukweni ya COSAFA baada ya kufanya vizuri katika mechi zake za leo Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Mechi ya kwanza Tanzania ilishinda 2-1 dhidi ya Comoro kabla ya kufungwa kwa penalti 4-3 na Msumbiji kufuatia sare ya 4-4 ufukwe wa South Beach Arena.
  Sasa Tanzania itamenyana na Angola katika mechi ya Nusu Fainali kesho hapo hapo South Beach Arena, wakati Msumbiji itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini katika Nusu Fainali nyingine.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATINGA NUSU FAINALI COSAFA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top