• HABARI MPYA

  Friday, November 26, 2021

  SAMATTA AIFUNGIA ANTWERP YATOA SARE UJERUMANI  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ameifungia bao la pili timu yake, Royal Antwerp ikitoa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya wenyeji, Eintracht Frankfurt katika mchezo wa Kundi D UEFA Europa League Uwanja wa Deutsche Bank Park Jijini Frankfurt, Ujerumani.
  Samatta alifunga dakika ya 88 baada ya kiungo Mbelgiji, Radja Nainggolan kufunga la kwanza dakika ya 33, wakati mabao ya Eintracht Frankfurt yalifungwa na Daichi Kamada dakika ya 12 na Gonçalo Paciência dakika ya 90.
  Kwa sare hiyo, Antwerp inafikisha pointi mbili na kuendelea kushika mkia, wakati Eintracht Frankfurt inafikisha pointi 11 na kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Olympiakos ya Ugiriki yenye pointi tisa na Fenerbahce ya Uturuki yenye pointi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AIFUNGIA ANTWERP YATOA SARE UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top