• HABARI MPYA

  Monday, November 01, 2021

  MBEYA KWANZA YALAZIMISHWA SARE NA POLISI

  WENYEJI, Mbeya Kwanza wamelazimishwa sare ya 2-2 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. 
  Mabao ya Mbeya Kwanza yamefungwa na Crispin Ngushi dakika ya 50 na Yahya Mbegu aliyejifunga dakika ya 53, wakati Polisi Tanzania na Tariq Seif dakika ya 24 na Vitalis

  Mayanga dakika ya 44. 
  Mbeya Kwanza inafikisha pointi sita baada ya mechi nne, wakati Polisi inafikisha pointi 10 katika mchezo wa tano na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA KWANZA YALAZIMISHWA SARE NA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top